Wed, 14 Aug 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Manchester United imethibitisha kukamilisha uhamisho wa walinzi Noussair Mazraoui (kulia pichani) na Matthijs de Ligt wote kutoka Bayern Munich ya Ujerumani kwa mkataba wa kudumu.
Mazraoui (26) raia wa Morocco ametua kwa ada ya Euro milioni 15 na nyongeza ya milioni 5 baadaye huku de Ligt (25) raia wa Uholanzi akijiunga kwa ada ya Euro milioni 45 na nyongeza ya milioni 5 baadaye.
Mabeki hao ambao wamewahi kucheza chini ya Meneja Eric Ten Hag wakati wakiwa Ajax wanaungana na kocha huyo huku de Ligt akisaini mkataba wa miaka mitano wakati Mazraoui akisaini mkataba wa miaka minne.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: