Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United ikijipata, mtajua hamjui

Man United Pata Man United ikijipata, mtajua hamjui

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United inapambana kuweka sawa kikosi chake kuhakikisha kinaanza kwa kishindo kwenye Ligi Kuu England na kuleta upinzani mkali kwenye mbio za ubingwa za kunasa taji hilo.

Jumamosi, Man United ilifikia makubaliano ya dili mbili na Bayern Munich kuwanasa mabeki Matthijs de Ligt na Noussair Mazraoui kwa ada ya pamoja ya Pauni 51.5 milioni. Hilo lilielezwa saa chache kabla ya Man United kuvaana na mahasimu wao Manchester City kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliofanyika uwanjani Wembley.

Alejandro Garnacho aliifungia Man United bao la kuongoza dakika za mwisho kabla ya Man City kusawazisha kupitia kwa Bernardo Silva na kufanya mechi hiyo kuingia kwenye hatua ya kupigiana mikwaju ya penalti ili kupata mshindi.

Jadon Sancho na Jonny Evans walikosa mikwaju yao ya penalti na kuinyima Man United fursa ya kubeba taji jingine baada ya kupoteza mchezo huo kwa penalti 7-6. Ilipofika Jumapili, Man United ilimshuhudia beki wake wa kulia Aaron Wan-Bissaka akitimkia zake West Ham United kwa ada ya Pauni 15 milioni na kinachoelezwa bado kuna wachezaji zaidi ya wawili wataingia Old Trafford na wengine zaidi wataachana na timu hiyo.

Ilielezwa Jumatatu, Man United ilikuwa bize kuwafanyia vipimo vya afya De Ligt na Mazraoui huko Carrington. Wakati huo, Wan-Bissaka naye alikuwa kwenye vipimo vya afya huko West Ham. Wan-Bissaka, 26 anaondoka na nafasi yake itazibwa na Mazraoui, ambaye pia anaweza kucheza kwenye beki ya kushoto.

Ripoti zinadai Man United ilirejea tena kwa kiungo Frenkie de Jong ikihitaji saini ya Mdachi huyo baada ya huko nyuma kujaribu mara kadhaa na kushindwa kumng'oa kutoka Barcelona. Sasa ripoti zinafichua Man United imepeleka ofa ya Euro 50 milioni ikihitaji saini ya mchezaji huyo, lakini Barcelona inaripotiwa kugomea ofa hiyo licha ya kuwa kwenye mkwamo mkubwa wa kiuchumi.

Kiungo Mbrazili, Casemiro anatarajia kubaki kwa msimu wake wa tatu Man United licha ya klabu za Saudi Arabia kuhitaji huduma yake. Kiungo huyo alikuwa kwenye kiwango cha ovyo sana msimu uliopita na kuna ripoti anaweza kuondoka Old Trafford kabla ya Agosti 30, siku ambayo dirisha la usajili litafungwa. Casemiro bado ana mkataba wa miaka miwili unaomshuhudia akilipwa Pauni 350,000 kwa wiki.

Chanzo: Mwanaspoti