Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yaingilia dili la Olmo Barcelona

Dani Olmo Man City yaingilia dili la Olmo Barcelona

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchestr City imewasilisha ofa nono RB Leipzig kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na timu ya taifa ya Hispania, Dani Olmo, 26, katika dirisha hili jambo linaloweza kusababisha mpango wa Barcelona kwa staa huyo kufeli.

Olmo mwenye umri wa miaka 26, anawindwa na timu nyingi Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga), pia katika michuano ya Euro akiwa na timu ya taifa ya Hispania ambapo timu ya kwanza kuripotiwa kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili ni Barcelona iliyoweka mezani Pauni 40 milioni, lakini ilikataliwa na Leipzig.

Mkataba wa sasa wa Olmo unatarajiwa kumalizika 2027 na kuna kipengele kinachomwezesha kuondoka ikiwa timu inayotaka huduma yake italipa Euro 60 milioni.

Olmo mwenyewe anaonekana kuwa na uhitaji zaidi wa kutua Barcelona badala ya Man City, lakini kuingia kwa Man City katika dili hilo kunaweza kusababisha aende upande mwingine kutokana na ofa nono ambayo timu hiyo inadaiwa kuiweka.

Msimu uliopita akiwa na Leipzig alicheza mechi 25 za michuano yote, akafunga mabao manane na kutoa asisti tano na kwenye Euro akiwa na Hispania alicheza mechi sita, akafunga mabao matatu na kutoa asisti mbili akiibuka mmoja kati ya mastaa waliochukua tuzo ya kiatu cha dhahabu.

Man City inataka kumsajili supastaa huyo kama sehemu ya kujiandaa na maisha bila kiungo, Kevin de Bruyne, ambaye anahusishwa na timu za Ligi Kuu Saudi Arabia.

Chanzo: Mwanaspoti