Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamba: Milango iko wazi kwenye nishati

Makama Waziri wa Nishati, January Makamba

Thu, 2 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Tanzania milango iko wazi kwenye uwekezaji wa sekta ya Nishati kutokana na uwepo wa mahitaji makubwa ya Nishati katika uzalishaji na Usambazaji kwenye maeneo ya sekta hiyo.

Waziri Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa Wadau wa sekta ya Nishati, Wawekezaji, Makampuni ya Nishati kutoka Nje, Mabalozi wa Nchi mbalimbali ambao unaangazia  hali ya sekta ya Nishati sambamba na maendeleo yaliyofikiwa, Mkutano ulioandaliwa na Energy Net Afrika. 

Waziri Makamba amesema "Kwanini Tanzania, kwanini sasa? Tanzania ni mahali sahihi penye amani katika kufanya uwekezaji, hivyo tunawakaribisha wawekezaji wenye tija kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini,".

Kwa upande wao washiriki katika mkutano huo wamepongeza juhudi za serikali katika sekta ya nishati kwa kufungua wigo wa Uwekezaji sambamba na kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo urasimu.

 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live