Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa, tutawarudisha nyumbali walioshindwa kutangaza utalii

25d956043a0829dcd8a3659cd4dc03d2.png?fit=550%2C400 Majaliwa, tutawarudisha nyumbali walioshindwa kutangaza utalii

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: dar24.com

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja sababu ya baadhi ya mabalozi kurejeshwa nchini muda mchache baadaya uteuzi kuwa ni kutokana na kushindwa kufanya chochote katika kutangaza utalii wa nchi.

Amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini nchini ambapo amesema kuwa serikali imetangaza mpango mahususi kwa ajili ya utalii wa nchi kwa mabalozi wote wa Tanzania ambapo imekuwa ni moja ya jukumu la mabalozi hao.

“Changamoto tuliyonayo ni baadhi ya mataifa kutangaza vitu vyetu kuwa ni mali yao, lakini tumeshaandaa mpango kupitia mabalozi wote wa Tanzania walioko kwenye nchi mbalimbali, moja kati ya jukumu lao ni kutangaza utalii wa nchi” amesema Waziri mkuu.

Ibada zarejea makanisani -DRC“Hatuwezi kukutambua kuwa wewe ni balozi wetu ukatutangaze alafu unakaa miezi mitatu au sita huna jambo la kufanya si bora urudi, wote wanajua na tunasimamia, kwahiyo mkisikia mtu ameenda na kurudi msishangae,” amesema Majaliwa.

Aidha, waziri mkuu amewakumbusha viongozi wanaopata fursa zakuzungumza mbele za watu kuacha maneno yenye kuondoa utu, dharau na hata  kuvunjiana heshima hususa ni kuelekea kipindi cha kampeni.

Uchaguzi Mkuu nchi Tanzania kufanyika Jumatano Oktoba 28 badala ya 25,ambapo Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa waliamua kufanya hivyo kutokana na kutambua mchango wa dini na kuondoa kero iliyokuwa ikijitokeza dakika za mwisho.

Video: Msemaji Mkuu wa Serikali awapatanisha Adamu na MbashaSADC kuimarisha mfuko wa dharula kupambana na majanga

Chanzo: dar24.com