Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo Alhamisi Septemba 26, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Kwanza, Rais Magufuli amemteua Profesa Blasius Nyichomba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Profesa Nyichomba ni Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Pili, Rais Magufuli amemteua Dk Rosemarie Mwaipopo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru. Dk Mwaipopo ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Tatu, Rais Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Nne, Rais Magufuli amewateua Rhoda Ngamilanga na Devotha Christopher Kamuzora kuwa Makamu Wenyeviti wa Baraza la Rufani za Kodi.
Tano, Rais Magufuli amemteua Profesa Yunus Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Profes Mgaya anashika wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mwili.
Pia Soma
- Majaliwa ataka wakuu wa idara kuwafuata wananchi vijijini
- Seth, Rugemalira wasota siku 828 gerezani
- Kupanda Mlima Kilimanjaro ni sawa na kwenda hospitali kuangalia afya
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi nchini Tanzania, Balozi John Kijazi imeeleza uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Septemba 26, 2019.