Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli amuwahisha kigogo mzito Yanga Mtwara

50034 JPM+PIC

Wed, 3 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

LEO Jumanne asubuhi kikosi cha Yanga kikiwa na mastaa wake 20 kitaanza safari kuelekea mkoani Mtwara, lakini kumbe ndani ya mkoa huo kuna ziara ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli na kigogo mmoja mzito wa Yanga, kumbe ziara hiyo ya Rais imemkuta huko akiandaa ramani ya ushindi wa timu yake.

Yanga itakutana na Ndanda ya Mtwara Alhamisi Aprili 4 pale Nangwanda Sijaona mchezo wa Ligi Kuu Bara, kumbe kigogo wake mzito kutoka kamati ya kusimamia timu hiyo iliyoundwa hivi karibuni tayari yuko eneo hilo kuanzia juzi.

Aliyetangulia huko ni Mwenyekiti wa Kamati, Lucas Mashauri, ambaye Mwanaspoti linafahamu kuwa tayari yuko Mtwara akiiwahi ziara ya Rais Magufuli ambaye ameanza ziara ya mkoa huo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mashauri ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati ya Usajili alisema kuwahi kwake mkoani humo kumetokana na ziara ya Rais Magufuli.

“Nani amekwambia mimi nipo huku? Ni kweli nipo huku lakini utaona nimewahi sana ni kutokana na kuhitajika kufanya hivyo kwani kuna ziara ya Rais Magufuli ambayo ataianza leo (jana),” alisema Mashauri

Mashauri alisema mbali na ziara hiyo haitakua ajabu akifanya pia maandalizi ya kuhakikisha timu yao inafikia sehemu salama na kuondoka na ushindi katika mechi hiyo.

Alisema zoezi hilo limetokana na kamati yao kugawana majukumu na kuhakikisha kabla ya timu yao kabla haijatua sehemu yoyote tayari kunakuwa na maandalizi mazuri kupitia usimamizi wa kamati yao.

“Unajua tumekubaliana kila timu yetu itakapokwenda ni lazima wajumbe wa kamati wawahi eneo hilo kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Lengo letu ni kuhakikisha jukumu tulilopewa linafanyika kwa weledi mkubwa.

“Tumegawana majukumu, unaona kuna waliokwenda Mwanza lakini mimi sikwenda nimekuja huku. Kwahiyo mpango huo utaendelea mpaka kamati yetu itakapolikabidhi jukumu kwa uongozi wa klabu utakaokuja.”

Mapema juzi kupitia Mwanaspoti Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Said Ntimizi, alifichua juu ya mpango wa kuhamasisha wachezaji wao kufanya vizuri na kwamba kila mchezo watakaoshinda wachezaji wao watajizolea kiasi cha Sh 10 milioni kama motisha na kuanza kutekeleza hilo katika mechi iliyopita ya Kombe la FA dhidi ya Alliance ya Mwanza.



Chanzo: mwananchi.co.tz