Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli amteua Mwinyi kuwa mkuu Muhas

77308 Pic+mwinyi

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) cha jijini Dar es Salaam.

Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania ameteuliwa kuendelea na wadhifa huo kuanzia leo Jumatano Septemba 25 2019.

Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa wenyeviti wanne wa bodi za taasisi mbalimbali kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua, Profesa Mayunga Nkunya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Profesa Nkunya anachukua nafasi ya Profesa Jacob Mtabaji ambaye muda wake umemalizika.

Profesa Nkunya ni Katibu mstaafu wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA).

Pili, Rais Magufuli amemteua, Profesa Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Rural Water Supply and Sanitation Authority – RUWASA).

Pia Soma

Advertisement
Profesa Mshoro ni Profesa wa Uhandisi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Tatu, Rais Magufuli amemteua, Profesa Elias Tozo Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Profesa Bisanda anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili.

Nne, Rais Magufuli amemteua Profesa Apollinaria Pereka kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Profesa Bisanda anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa wenyeviti hao umeanza leo Septemba 25, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz