Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lule kuongeza nguvu Ihefu

Luleeeeeee Aliyekuwa kocha msaidizi wa Singida Fountain Gate, Mathias Lule

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Singida Fountain Gate, Mathias Lule leo amejiunga katika kambi ya klabu ya Ihefu.

Ihefu imeweka kambi Jijini Arusha kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Lule tayari ameshajiunga nayo kuongeza nguvu katika benchi la ufundi.

Habari ambazo Mwanaspoti imepenyezewa, kocha huyo amejiunga na Ihefu leo asubuhi na kinachosubiriwa ni kutambulishwa.

Wakati Lule anawasili katika kambi hiyo, inaelezwa kwamba wapo wachezaji wa kigeni kutoka nchini DR Congo ambao nao watatambulishwa muda wowote kuanzia sasa.

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo kililidokeza Mwanaspoti Online kwamba Lule anasubiriwa kutangazwa muda wowote.

“Lule yupo huku nadhani watamtangaza muda wowote ule, benchi la ufundi linajipanga ili kuleta ushindani kwenye Ligi,” kimesema chanzo hicho.

Ujio wa Lule unaenda kuboresha benchi la ufundi baada ya timu hiyo awali kumtambulisha Mecky Maxime kuwa kocha wao mkuu akirithi mikoba ya Moses Basena aliyetupiwa virago.

Timu hiyo hivi karibuni ilitangaza kubadili menejimenti, benchi la ufundi na kufanya usajili wa wachezaji ili kuhakikisha inajinusuru kushuka daraja.

Ihefu hadi sasa inashika nafasi ya 13 ikicheza mechi 14, imeshinda tatu, sare nne na kufungwa saba na kujikusanyia pointi 13.

Chanzo: Mwanaspoti