Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#LIVE: Kamati ya maadili TFF yamfungia manara miaka 2, Faini Milioni 20

Video Archive
Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lile Sakata lililokuwa likimuhusisha Msemaji wa Yanga, Haji Manara kuhusu kumtishia na kumdhalilisha Rais wa TFF Wallace Karia Julai 2 mwaka huu katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Azam Sports.

Sasa leo Julai 21, Kamati ya Maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Wakili Mwita Waisaka, imeeleza kuwa imemtia hatiani Msemaji huyo wa Yanga na kumpa adhabu ya kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na nje ya Tanzania kwa muda wa miaka miwili.

Mbali na kifungo hicho Manara amepigwa Faini ya Milioni 20, na adhabu hiyo itaanza leo Julai 21, 2022.

Adhabu hizi zimetolewa kwa mujibu wa kifungu 73.5 na 73.6 za kanuni za maadili za TFF toleo la mwaka 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live