Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha TS Galaxy: Aziz Ki, Aucho, Diarra ni watu hatari pale Yanga

Aziz Ki Diarra Kocha TS Galaxy: Aziz Ki, Aucho, Diarra ni watu hatari pale Yanga

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya TS Galaxy ya nchini Afrika Kusini, Sead Ramovic amesema kuwa Klabu ya yanga inao wachezaji bora barani Afrika, wenye uwezo na maarifa makubwa ya kuifanya timu iweze kupata matokeo wakati wowote na kuamua mechi.

Sead Ramovic ambaye ni raia wa Ujerumani amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki wa Mpumalanga CUP kati ya galaxy dhidi ya Yanga ambapo Wananchi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na mshambuliaji Prince Dube dakika ya 55.

“Ilikuwa mechi nzuri dhidi ya Yanga ambayo ni timu kubwa, wana kocha mkubwa, hivyo ilikuwa jambo kubwa kwetu kupata mechi kama hii na kupata kile tulichokipata. Bado tuna mchezo mmoja dhidi ya Augsburg ambao naamini ututaendelea kupata fitness zaidi kabla ya ligi kuanza ambapo tunatarajia tutakuwa na utimamu wa asilia 100.

“Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri japo kulikuwa na makosa machache, tunatakiwa kuboresha tuongeze kasi, kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko na sisi tulifanya mabadiliko lakini wenzetu walikuwa bora zaidi, walicheza vizuri zaidi yetu na kupata ushindi. Huu ni mchezo wa kirafiki kwa hiyo tunatazama zaidi mambo muhimu ya kuboresha kwenye kikosi chetu.

“Yanga ina wachezaji wakubwa Afrika, top players kama wanne ama watano, yupo Aziz Ki, Khalid Aucho na kipa Djigui Diarra, hawa ni baadhi tu, Yanga ni timu bora sana. Niliwatazama wakati wanacheza na Mamelodi Sundowns na walikuwa karibu kupata ushindi lakini hawakuwa na bahati tu, wana kocha mzuri, uongozi mzuri chini ya Eng. Hersi, jamaa ni mtu sana, ninaamini watafanya makubwa sana kwenye michuano ya CAF msimu huu,” amesema Sead Ramovic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live