Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa mwanae, Rais Museveni awaomba radhi Wakenya

Aa0bc8e3 B0b5 40b4 A1c3 4b1c90035256 Rais Museveni na Muhoozi

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaomba radhi wananchi wa Kenya na Wana-Afrika Mashariki kwa ujumla kufuatia mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuandika kwenye mtandao Twitter kauli ambazo zililenga kuvuruga uhusiano wa kidiplomasia ikiwemo kauli ya kutaka kuiteka Nairobi na kumtaka Uhuru Kenyatta agombee muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Rais Museveni amesema haikuwa sahihi kwa Muhoozi ambaye alikuwa Mkuu wa Jeshi la Ardhini la Uganda kabla ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo jana, kuandika alichokiandika na kusema ule haukuwa msimamo wa Serikali ya Uganda.

Museveni ametolea ufafanuzi pia sababu za kumpandisha cheo Muhoozi kutoka Luteni Jenerali na kumpa cheo cha Ujenerali licha ya kauli zake hizo tata ambapo amesema pamoja na kosa hilo, lakini Muhoozi anayo mazuri mengi na mchango mkubwa alioutoa na anaoweza kuendelea kuutoa.

“Nimetumia utaratibu wa kuoneshwa kutopendezwa na mabaya huku wakati huohuo nikimtia moyo Muhoozi kwa mazuri yake.

“Samahani sana ndugu zetu Wakenya na eatu wa Uganda ambao mlikwazwa na kauli za Muhoozi, mbali na ombi hili la wazi nimewasilisha pia samahani yangu nyingine ya siri kwa Rais wa Kenya, William Rutto.”



Chanzo: www.tanzaniaweb.live