Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo cha Robert Mugabe, Rais Magufuli atangaza siku tatu za maombolezo

74617 MAGU+PIC

Sat, 7 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Rais mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe, Robert Mugabe (95) kilichotokea leo Septemba 6, 2019 nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika siku tatu za maombolezo zinazoanzia leo Ijumaa hadi Jumapili ya Septemba 8, 2019 bendera za Tanzania zitapepea nusu mlingoti.

Taarifa iliyotolewa  leo usiku Ijumaa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania imesema Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, familia ya Mzee Mugabe, wananchi wa Zimbabwe, Waafrika na wote walioguswa na msiba huo.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Gabriel Mugabe.”

“Afrika imepoteza mmoja wa viongozi jasiri, shupavu, mwanajumuiya wa Afrika (Pan-Africanist) na aliyekataa ukoloni kwa vitendo, Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”

Rais Magufuli ameongeza kuwa Hayati Robert Mugabe aliipenda Tanzania, alijenga uhusiano na ushirikiano wa karibu, kidugu na kirafiki na Tanzania tangu enzi za uongozi wa Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwamba Afrika itamkumbuka kwa jinsi alivyoshirikiana na viongozi mbalimbali kupinga ukoloni na ukandamizaji wa haki za Waafrika.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement


Chanzo: mwananchi.co.tz