Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Denis aikimbia nchi, atoroka na Pesa za Simba SC (+Video)

Video Archive
Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Ubaya Ubwela, mambo yanazidi kuvurugika katika kambi ya Simba baada ya sakata la kiungo wake Mshambuliaji Kibu Denis Prosper kuchukua sura mpya”.

Kibu Denis ambae hajaonekana katika kambi ya Simba inayojiandaa na maandalizi ya msimu mpya 2024/25 nchini Misri, Jioni ya leo Julai 23 kumezuka taarifa mpya ambazo huenda zikawa ni za kushtua wapenzi na Mashabiki wa Timu hiyo.

Mwandishi na mchambuzi nguli wa Habari za Michezo nchini, Jemedari Said Kazumari, kupitia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, ametoa taarifa inayoonesha kuwa Kibu huenda amewatoroka Simba na kutimkia nchini Norway,Jemedari ameandika:

Mchezaji wa Simba SC, KIBU DENIS PROSPER ameitoroka timu yake ya Simba jioni ya leo na kukimbilia nchini Norway. Kibu ambaye amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka 2 na kupokea kiasi cha Shilingi za Kitanzania Milioni 400 ameondoka na ndege ya Ethiopia Airline ya saa 10 jioni kupitia Addis Ababa akitumia tiketi ya kwenda pekee (single ticket) bila na kuwa na ya kurudia hali inayotia shaka kwamba huenda asirudi tena nchini.

Mchezaji huyo Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Demokrasi Congo ambaye alipata uraia wake miaka michache iliyopita ameitia hofu klabu yake kwamba huenda anaenda “KUJILIPUA” kama mkimbizi na asirudi tena ilihali ameshachukua milioni 400 na amekosekana kambini tangu Simba imeanza Pre-season.

Wakala anaetambulika na klabu wa mchezaji huyo ambaye Bin Kazumari imetambulishwa kwa jina moja la Yazidu (Mwanasheria) alishapokea mkwanja wake na kusaini karatasi za mkataba na malipo na klabu kitambo, huku katika hali nyingine Simba wakionekana kumkana mtu mwingine yoyote ambaye sio Yazidu kujitangaza kama wakala wa Kibu na wametia shaka huenda kuna mtu yuko nyuma ya mpango wa kumtorosha mchezaji.

Picha 3 ni KIBU alivyopita airport “Kininja”, nyingine inaonyesha Visa na mwisho ni passport yake. Simba inafanya jitihada kuhakikisha kijana wao anarejea kambini kujiunga na wenzake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: