Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mpina dhidi ya mawaziri wawili kuunguruma leo

Mpina Mwwww Kesi ya Mpina dhidi ya mawaziri wawili kuunguruma leo

Wed, 18 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina dhidi ya Waziri wa Kilimo, Waziri wa Fedha na taasisi saba zikiwamo kampuni, inatarajiwa kusikilizwa leo Jumatano Septemba 18, 2024.

Shauri hilo la Kikatiba namba 18383/2024 linatarajia kusikilizwa katika Mahakama Kuu, Masjala ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Anold Kirekiano, imepangwa kuanza saa nane mchana mahakamani hapo.

Katika shauri hilo, Mpina, anapinga uamuzi wa Waziri wa Kilimo kutoa vibali vya ununuzi wa sukari kupitia Bodi ya Sukari kwa kampuni ambazo hazimiliki viwanda vya sukari wala sukari.

Pia, anapinga Waziri wa Fedha kuruhusu Kamisha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuamuru kampuni za vocha kuingiza sukari nchini bila kulipa kodi na kusababisha Serikali kupoteza mapato ya Sh1.548 bilioni.

Mpina pia, ameshtaki kampuni za sukari kwa kukubali kuingiza sukari na kupewa msamaha wa kodi.

Mbali na mawaziri hao, wajibu maombi wengine ni Bodi ya Sukari, Kampuni ya Itel East Africa Limited na Zenj General Merchandize, na mwanasheria mkuu wa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live