Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanuni 3 za kukusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa

98 Shopping 2597135k 660x400

Tue, 12 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Kila mtu huwa na njia yake ya kutafuta pesa na kila mtu huwa anajipangia atumie vipi mkwanja wake lakini huwa tunatofautiana kwenye jinsi ya kutumia hizo pesa…

AyoTV na millardayo.com kwenye pitapita zimekutana na hizi kanuni tatu au mambo matatu ambayo yanaweza kukusaidia kuwa na matumizi mazuri ya pesa wakati wote.

1. Fikiria na ujiulize ni kweli unakihitaji kitu unachotaka kukinunua?

Katika hili ni vizuri ukajiuliza kwanini unataka kununua hicho kitu na kutafakari kama kweli kina umuhimu kwa wakati huo au la, pia ni vyema kujiuliza gharama unayoitumia kununua kitu na huduma hiyo inafanana na ubora wa kitu chenyewe na kwa muda gani kitu hicho kitadumu?

Unatakiwa pia kujiuliza kama hicho kitu kinaweza kuwa sababu ya wewe kujipatia kipato kingine, kama kinaweza kufanya hivyo basi sawa unaweza kukilipia.

2. Punguza kiwango cha pesa unachotembea nacho kwenye pochi au wallet yako.

Kwa kutembea na pesa unaweza kujikuta unaingia gharama za kununua vitu ambavyo hukuwa na mpango wa kuvinunua na hapa unashauriwa kuhakikisha unatunza pesa zako Benki na unapotoka kwenda kwenye mizunguko ya kawaida ni vizuri ukachukua kiwango maalumu kwa ajili tu ya matumizi.

3. Kanuni ya “Fanya mwenyewe”

Hii inamuhitaji mtu mwenyewe kutafakari vitu gani anaweza kuvifanya mwenyewe na badala yake anatoa pesa ili vifanywe na watu wengine.

Si vibaya kwenda kutengenezwa kucha au kutengeneza nywele saluni  lakini pia sio vibaya kujifunza kujipaka rangi au kujiosha nywele mwenyewe na huduma nyingine zinazoendana na hizo ili kuweza kuzifanya mwenyewe na wakati mwingine kutumia hela ambayo ingetumika kwenye mambo haya sehemu nyingine.

Kwa upande mwingine tabia ya kula migahawani husababisha matumizi makubwa sana ya fedha ambayo huweza kuepukwa kwa kujijengea tabia ya kupika nyumbani wewe mwenyewe pale inapowezekana.

Ulipitwa na hii? Alichofanya JOTI baada ya Babu Seya na Papi Kocha kuachiwa huru

Chanzo: millardayo.com