Wed, 14 Aug 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Israel Mwenda amesaini mkataba wa miaka mitatu na Klabu ya Singida Black Stars baada ya kukubaliwa ombi lake la kuondoka katika klabu ya Simba SC.
Mwenda mwenye umri wa miaka 24 amesaini Singida baada ya kuilipa fedha Simba Sports Club kama walivyokubaliana baada ya kuomba kuondoka klabuni hapo.
Israel Mwenda ambaye ametumika kwa miaka mitatu ndani ya kikosi cha Simba, alitakiwa alipe fedha ili aachiwe huru kwenda sehemu yoyote.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: