Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iddi Nado azipigia hesabu Simba na Yanga

Nado Azam Ns Iddi Nado azipigia hesabu Simba na Yanga

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa Azam FC, Idd Suleiman (Nado) amebainisha kuwa kwa muda mrefu hajazifunga timu kubwa jambo ambalo anaomba Mungu litimie msimu mpya.

Ni Agosti 16 2024 msimu wa 2024/25 unatarajiwa kuanza ambapo mabingwa watetezi ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Mechi kubwa dhidi ya Simba na Yanga Nado hakupata nafasi kufunga kwenye mechi ambazo walikutana uwanjani kusaka ushindi.

Ipo wazi kwamba Azam FC msimu wa 2023/24 iligotea nafasi ya pili itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika itaanzia hatua ya awali. Nado amesema: “Sijapata nafasi ya kufunga kwenye mechi kubwa kwa muda mrefu hivyo hilo ninapenda kuona likitokea kwenye mechi za ushindani nina amini itakuwa hivyo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live