Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hojlund apewa jezi ya Martial

Rasmus Hojlund 9 Hojlund apewa jezi ya Martial

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imethibitisha Rasmus Hojlund atavaa jezi Na 9 msimu ujao iliyoachwa na Anthony Martial aliyeondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Hojlund alichukua muda kuzoea mazingira United baada ya uhamisho wake uliogharimu Pauni 72 milioni akitokea katika klabu ya Italia ya Atalanta mwaka jana.

Staa huyo, 21, aling’ara katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga mabao matano ya hatua ya makundi, lakini kwenye Ligi Kuu England alianza kwa taabu akihitaji mechi 15 ili kufunga bao lake la kwanza EPL.

Mabao zaidi yakafuata na kumfanya Hojlund kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga katika mechi sita mfululizo za EPL na kumaliza msimu wake wa kwanza akifunga mabao 16 katika michuano yote.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark alianza maisha United akivaa jezi Na 11 ambayo zamani ilivaliwa na Ryan Giggs, wakati Anthony Martial alibaki na Na 9.

Martial aliondoka klabuni hapo mwisho wa msimu baada ya United kuamua kutomuongeza mkataba, hivyo Hojlund sasa amechukua jezi hiyo.

Amerejea mazoezini pamoja na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa Christian Eriksen baada ya Denmark kushiriki michuano ya Euro 2024.

Aidha, Joshua Zirkzee – ambaye amesajiliwa United amepewa jezi Na 11.

Chanzo: Mwanaspoti