Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hanspope, Dk Msolla na Kibadeni watoa neno usajili Simba, Yanga

Kibadeni+pic Hanspope, Dk Msolla na Kibadeni watoa neno usajili Simba, Yanga

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroKocha wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni ameuzungumzia usajili wa timu za Simba na Yanga katika dirisha hili, huku vigogo wa timu hizo, Zacharia Hanspope na Dk Mshindo Msolla wakianika mipango ya klabu zao.

Mpaka sasa Simba imewasajili Bernard Morrison, Lally Bwalya, Chrispin Mugalu, Joash Onyango, Ame Ibrahim, Ilanfya Charles na David Kameta ‘Duchu’.

Kwa upande wake, Yanga imewasajili Sogne Yacouba, Bakari Mwamnyeto, Yassin Mustapha, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Kibwana Shomari, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonobe.

Kibadeni, nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars amewashauri wachezaji wazawa kutoridhika kuwekwa benchi na wageni, ili wajiuze vizuri katika soko la wachezaji.

“Usajili wa Simba na Yanga kwa kiasi fulani umetikisa, lakini ligi itakapoanza ndipo tutaona kama tunachoaminishwa sasa ndicho kimefanyika katika viwango hasa kwa wageni,” alisema jana katika mahojiano na Mwananchi.

“Lakini kinachonisikitisha ni wachezaji wetu wa nyumbani, tunafahamu sasa mpira ni biashara, wazawa wanapaswa kupambana kila mmoja ajitambue kwani soka ni soko huria, wasiridhike kuwekwa benchi, wajitume.”

Chanzo: mwanaspoti.co.tz