Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fountain Gates yaja kivingine msimu wa 2024-25

Singida XIe.jpeg Fountain Gates yaja kivingine msimu wa 2024-25

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Fountain Gates yenye makao makuu mkoani Manyara imejipanga vyema kuelekea msimu huu baada ya kukamilisha sajili za wachezaji wake wote itakaowatumia.

Fountain Gate wametoa majina ya wachezaji 32 ambao kati ya hao wachezaji watano ni vijana na 27 watatumika zaidi msimu huu.

Klabu hiyo itacheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Namungo huko Lindi Majaliwa Stadium tarehe 17 na mchezo wa pili itacheza dhidi ya Simba tarehe 25 Agosti katika dimba la KMC Complex jijini Dar es salaam.

Klabu hiyo itarejea dimba lake la nyumbani la Tanzanite Kwaraa dhidi ya Ken Gold tarehe 11 September na mchezo dhidi ya Dodoma jiji tarehe 15. Fountain Gates si wageni wa ligi kuu bali wamebadili jina.

Msimu wa 2021/22 walipanda daraja na walijiita Singida Big Stars na msimu wa 2023/24 walibadili jina na kujiita Singida Fountain Gates baada ya klabu hiyo kuuzwa na kuchukuliwa na mmiliki mwingine. Msimu wa 2024/25 klabu hiyo imebadili jina na sasa inaitwa Fountain gates.

Hiki hapa kikosi cha Fountain gates msimu wa 2024/25

Chanzo: www.tanzaniaweb.live