Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fatma Karume: TFF wanakosea, maamuzi yetu ni CAS

Fatma Karume X Fei Sio Mtumwa Fatma Karume ameweka wazi kuwa atamshauri Feisal wapeleke kesi Mhakama ya CAS

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jana Machi 2, Kamtai ya Sheria na hadhi za Wachezaji ya TFF kupigilia msumari katika sakata la Kiungo wa Yanga Feisal Salum (Fei Toto) kuwa bado ana Mkataba halali na Yanga wakityupilia mbali mapitio ya rufaa aliyoomba Feisal.

Wakili wa mchezaji huyo , Mwanamama Fatma Karume amesema wanachofikiria sasa ni kwenda CAS ili kutafuta haki ya mteja wake.

Katika maelezo yake Fatma anaonekana kuwashambulia TFF kwa kumlazimisha Fei Toto kufanya kazi na Yanga jambo ambalo analipinga akidai kuwa Feisal sio mtumwa ana uhuru wa kuchagua sehemu ya kufanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria za mchezo wa mpira wa miguu.

Akizungumza Fatma anasema;

"...Tunasubiri nakala ya hukumu kutoka TFF na kisha nitamshauri Fei Toto kama maamuzi yake yatabaki hivyo tutaenda CAS.

Tatizo la TFF ni kumlazimisha Fei Toto kucheza Yanga kinyume na sheria za FIFA.. huwezi kumlazimisha mchezaji kucheza Yanga sio mtumwa yule.

Kama Yanga wanajua Fei Toto kavunja Mkataba kinyume na utaratibu, maana yake tayari mkataba haupo hivyo TFF wanatakiwa kutoa adhabu kama ni faini au kufungiwa miezi minne kwa mujibu wa sheria za FIFA na sio kumlazimisha mchezaji kucheza Yanga sio mtumwa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live