Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, ameonekana kuridhishwa na namna timu hiyo inavyocheza huku akisema ubora ulioonyeshwa katika mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii ndiyo unaotakiwa ndani ya Yanga.
Hersi amebainisha kwamba, katika kipindi cha usajili ambacho kinaelekea ukingoni, wameshusha wachezaji ambao wamekuwa na msaada mkubwa kikosini hapo akiwemo Chadrack Boka ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Joyce Lomalisa aliyeondoka.
“Tumekuwa na mabadiliko mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa na tija kikosini, hii inatufanya sisi viongozi kufurahia mafanikio ambayo tunaendelea kuyapata ingawa tunatambua bado tuna safari ndefu katika michuano ya kimataifa.”