Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eng. Hersi athibitisha; Azi Ki hajasaini, uwezekano wa kubaki ni 60%

Video Archive
Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa kiungo nyota wa timu hiyo, Stephane Aziz Ki bado hajasaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo ingawa wapo katika nafasi nzuri ya kumbakisha.

Akizungumza nchini Afrika Kusini jana Julai 8, 2024, Hersi amesema kuwa klabu inapambana kwa juhudi kubwa kumshawishi mchezaji huyo abakie na yeye mwenyewe anaonyesha dalili za kutamani kubaki ingawa nguvu ya fedha inaweza kumuondoa.

“Ni mkakati wa klabu kuhakikisha mchezaji anabaki na majadiliano yanaendelea vizuri na hapana shaka tutarudi kufanya utambulisho ingawa kuna klabu nyingi zinamhitaji mchezaji.

“Hivyo majadiliano yanaendelea na ninaweza kusema kuna nafasi kubwa kwa mchezaji kubakia lakini hatujakamilisha.

“Aliweka wazi kuwa anataka kubaki unajua nilimsaini miaka miwili iliyopita na nilimsajili kutoka Asec Mimosas na nikamueleza kuhusu ‘project’ yangu na nani nataka waipeleke klabu katika ngazi za juu na akawa sehemu muhimu ya program na mpango ambao upo hi vyo majadiliano yakawa yaleyale na alisema wazi kuwa nahitaji kubaki hapa na kuipeleka Yanga katika ngazi ambazo unataka ifike.

“Lakini mpira ni biashara sasa unaweza kusema unataka kubaki lakini hali ya kifedha ikabadilisha mawazo kwa hiyo naweza kusema ni 60/40 (uwezekano wa kubaki),” alisema Hersi.

Ki alitoa mchango mkubwa kwa Yanga msimu uliopita ilipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ambapo aliibuka kinara wa kufumania nyavu akipachika mabao 21 na assists 8. Idadi hiyo ya mabao ilimuwezesha nyota huyo kutoka Burkina Faso kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu.

Msimu wake wa kwanza kuichezea Yanga ambao ni 2022/2023, Aziz Ki alitoa mchango mkubwa katika kuiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tetesi kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa Aziz Ki bado hajamwaga saini, sababu ikitajwa ikiwa ni kushindwa kutekelezewa mahitaji aliyowasilisha mezani ili kuongeza mkataba mpya.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya Yanga, Aziz Ki anataka alipwe mshahara wa kiasi cha Dola 18,000 (sawa na Sh 47 milioni za Kitanzania) kwa mwezi na ofa ya Yanga ni dola 12,000.

Kete pekee Yanga wanayoitegemea ni vigogo wawili ndani ya Klabu hiyo, ambao wanatarajiwa kukutana na menejimengi ya Aziz Ki ambaye anarejea leo nchini ili wajaribu kumbakisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live