Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ebola: Museveni awapiga 'Stop' waganga wa jadi

MUSEVENI WEB Museveni awapiga 'Stop' waganga wa jadi

Thu, 13 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewaagiza waganga wa kienyeji kusimamisha kazi zao zote na kuwahudumia wateja wakati wa mlipuko wa Ebola.

Katika hotuba yake kwa taifa iliyoonyeshwa kwenye televisheni, alitumia lugha ya Kiganda inayozungumzwa na watu wengi, aliwaambia waganga wa kiroho na waganga wa mitishamba wasijihusishe na kujaribu kuwatibu watu wanaoshukiwa kuambukizwa ugonjwa wa ebola.

Hii inafuatia kifo cha mzee wa miaka 45 ambaye alikuwa ameorodheshwa na maafisa wa afya kuwa ameambukizwa virusi vya ebola.

Mwanamume huyo, ambaye alifariki katika hospitali ya Kampala mnamo Oktoba 7, alikimbia kutoka kijijini kwake wilayani Mubende, kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo, alitafuta matibabu kutoka kwa mkuu wa jadi katika mkoa mwingine, kabla ya kufika katika hospitali hiyo katika mji mkuu.

Alikufa baada ya takriban masaa kumi ya kulazwa hospitalini, mamlaka inasema.

Baadhi ya wanafamilia wa mwanamume huyo wamewekwa chini ya karantini, wakati wengine walijificha kutoka kwa wafanyikazi wa matibabu. Rais aliwataka kuripoti katika vituo vya afya.

Ingawa Bw. Museveni alisema kwa sasa hakuna kesi zilizothibitishwa za Ebola mjini Kampala, alionya umma kuendelea kuwa waangalifu, na kutoa hakikisho kwamba wahudumu wa afya watadhibiti janga hilo.

Rais pia aliamuru huduma za usalama zinazofanya kazi pamoja na maafisa wa afya kuwakamata watu wanaoshukiwa kuwa na virusi ambao wanakataa kutengwa kwauchunguzi zaidi.

Imepita karibu mwezi mmoja tangu mlipuko wa Ebola ya Sudan kutangazwa nchini Uganda, ambayo imeenea katika wilaya tano. Kufikia sasa, watu 54 wamethibitishwa kuwa na virusi, huku vifo 19, vikirekodiwa.

Watu 20, wakiwemo wafanyikazi watano wa matibabu, wamepona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live