Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EPL kuishitaki FIFA

Hytdytfydd EPL kuishitaki FIFA

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu England na chama cha wanasoka wa kulipwa (PFA) ni kati ya makundi yaliyoungana na kujipanga kulishitaki shirikisho la soka la kimataifa (FIFA) kwa kupanga kalenda za mechi za kimataifa ambazo ni hatari kwa afya za wachezaji.

Malalamiko hayo ya pamoja yanaonyesha kwamba bodi hiyo ya soka inatumia vibaya mamlaka yake kuathiri afya za wachezaji kwa kupanga ratiba ambazo sasa ‘zinaumiza'.

Lakini FIFA imezijibu vikali baadhi ya ligi, likizituhumu kwa kuwa na 'upuuzi mwingi' na 'zinafanya mambo kwa maslahi binafsi ya kibiashara' kwa kuandaa ziara za mwisho wa msimu za kusaka pesa.

Ligi hizo za Ulaya, zinasema FIFA inaathiri 'mikakati ya kiuchumi ya ligi za ndani na afya za wachezaji'.

Pia muungano huo unasema FIFA kuwa kama msimamizi na pia muandaaji wa michuano inaleta mgongano wa kimaslahi.

FIFA inatuhumiwa kushindwa kuomba ushauri katika mabadiliko iliyoyafanya hivi karibuni katika kalenda, ikiwamo kuanzisha michuano mipya ya Kombe la Dunia la Klabu litakalojumuisha timu 32 kati ya Juni na Julai mwakani.

“AFCON badala yake itachezwa katikati ya msimu wa ligi za Ulaya. Hii itaathiri moja kwa moja ligi za ndani, klabu na - kubwa zaidi - afya za wachezaji (miili yao itatumika kupitiliza),” alisema mtendaji mkuu wa PFA, Maheta Molango.

Msemaji wa FIFA alisema juzi: “Kalenda ya sasa ilipitishwa kwa pamoja na Baraza la FIFA, ambalo linajumuisha wawakilishi kutoka mabara yote, likiwamo la Ulaya, na limekusanya maoni ya kina kutoka kwa vyama vya soka na FIFPRO.

“Kalenda ya FIFA ipo kuhakikisha soka la kimataifa linaendelea kuwepo, lisife na likue sambamba soka la klabu.”

Chanzo: Mwanaspoti