Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dube: Ninaahidi makubwa Yanga - Video

Video Archive
Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube amesema kuwa anafurahia kusajiliwa na Klabu hiyo kwani ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu kucheza soka kwenye klabu kubwa kama Yanga.

Dube amesema hayo leo wakati akiondoka na Kikosi cha Yanga kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Toyota Cup na michezo mingine ya kirafiki ambayo wamealikwa na kaizer Chiefs.

“Nafurahi kucheza Yanga, nafurahi kucheza na Chama na Aziz Ki, kuna wachezaji wakubwa hapa na kila mchezaji anatamani kucheza Yanga ili ushinde makombe. Ilikuwa ndoto yangu kucheza timu kubwa na nipo hapa kwa ajili ya kufanya kazi.

"Nimepitia kipindi kigumu na sasa natamani kufurahi na kuitumika klabu yangu ya sasa. Mambo yanakwenda vizuri, nimekaribishwa vizuri kuanzia kwa mashabiki, viongozi, na benchi la ufundi na kila mtu na najisikia furaha.

"Nipo hapa kuongeza nguvu kwenye timu yetu ya Yanga ili tuweze kushinda makombe. Ni timu yenye mashabiki wengi wamenionesha upendo na makaribisho makubwa, siku ya Wananchi waje kushuhudia mambo makubwa. Mimi nipo tayari kuwafurahisha na kama nitakuwa timamu kimwili kwenye kila mchezo," amesema Prince Dube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live