Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Doumbouya aikataa demokrasia ya Magharibi Baraza Kuu UN

Mamady Doumbouya1 Doumbouya aikataa demokrasia ya Magharibi Baraza Kuu UN

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea, Kanali Mamady Doumbouya ametetea mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika katika baadhi ya nchini za Afrika akisema kuwa kuwa mfumo wa demokrasia wa Magharibi haufanyi kazi kwenye bara hili.

Ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuwa Afrika imekuwa ikitaabika na mfumo wa demokrasia ambao umelazimishwa kwao na ambao unapata wakati mgumu kuendana na mazingira.

"Ni wakati sasa mwache kutufundisha na kutuchukulia sisi kama watoto," amesema Doumbouya ambaye alitwaa madaraka mwaka 2021 baada ya kumpindua Rais Alpa Conde.

Amesema mapinduzi aliyoyafanya yalikuwa ni lazima ili kulinda machafuko zaidi nchini humo, ambapo maelfu ya wananchi wa Taifa hilo walipokea mapinduzi hayo kwa furaha baada ya Rais Conde kuondolewa.

Guinea ni moja ya nchi za Afrika ya Kati na Magharibi ambazo zimeshuhudia mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya karibuni, nyingine zikiwa ni pamoja na Mali, Burkina Faso, Niger na Gabon.

Mapinduzi hayo yamekuwa yakikosolewa vikali na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Umoja wa Mataifa (UN).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live