Sharif Abdallah Ali, mdogo wa marehemu Ali Kibao, ameeleza kuhusu uamuzi wa familia kutokana na kifo cha ndugu yao.
Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu, Amos Makalla amesema hayo akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
“Nimeona kwenye Vyombo vya Habari kuanzia asubuhi mpaka sasa nitoe pole kwa Chama cha Chadema kwa kumpoteza mmoja wa Wajumbe wa Sektarieti bwana Ali Kibao nimekuwa nikifuatilia sisi ni vyama vya siasa linapokuja suala la ubinadamu Chama unaweka pembeni, nawapa pole kwa msiba”
“Mimi niombe Jeshi la Polisi likatimize wajibu la kuendelea na uchunguzi wa jambo huo , na katika hili sisi ni binadamu, utu na ndio mana nimesimama hapa kutoa pole kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi,”
Kibao alikuwa ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho ambapo siku chache zilizopita, ilidaiwa kwamba ametekwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya basi, akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga.
Muda mfupi baadaye, ndipo zilipopatikana taarifa kwamba mwili wake umeokotwa katika Viwanja va NSSF, Ununio jijini Dar es Salaam na baadaye kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mwananyamala.