Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Yanga yamtambulisha Chama - VIDEO

Video Archive
Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetangaza kumsajili Kiungo Mshambulia, Clatous Chota Chama raia wa Zambia akitokea Klabu ya Simba.

Chama anajiunga na Yanga akiwa Mchezaji Huru baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia Simba ambayo ameitumikia katika vipindi viwili tofauti.

Klabu yetu ya Young Africans imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji Clatous Chama raia wa Zambia.

Chama ambaye kiwango chake kimekuwa kivutio machoni mwa watazamaji amejiunga na timu yetu akitokea kwa watani zetu wa jadi hapa nchini.

Kiungo huyo ambaye ana uzoefu na soka la Tanzania, alianza kuonyesha uwezo wake hapa nchini mwaka 2018 alipotua kwa mara ya kwanza.

Ujio wa Chama katika kikosi chetu unaongeza wigo mpana katika eneo la kiungo cha ushambuliaji akiwa sambamba na Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki.

Taarifa ya Yanga; "Haya ni maboresho ya kikosi chetu katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa kuelekea msimu ujao wa 2024-2025 tukiwa na malengo ya kutetea mataji yetu yote tuliyobeba msimu wa 2023-2024 ambayo ni Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank Federation huku pia tukihitaji kufanya vizuri zaidi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuishia robo fainali msimu uliopita.

Huu unakuwa usajili wa kwanza kukamilika huku pia maboresho zaidi yakiendelea. Kaa tayari Mwananchi kwa ajili ya kufurahi zaidi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live