Wed, 14 Aug 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Msemaji wa Timu ya Vital’O ya Burundi, Arsene Bucuti @arsene_bucuti amesema iwapo Yanga itaifunga Vital’O kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa atajiuzulu kuwa msemaji wa timu hiyo.
Bucuti ameyasema hayo kwenye kipindi cha radio cha Sports Arena cha Wasafi FM.
"Mimi Young Africans akinifunga nitajiuzuru, mechi ya kwanza tu akinifunga naachia ngazi," amesema Bacuti.
Vital’O itawaalika Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Agosti 17, 2024 kwenye Dimba la Azam Complex, Dar es Salaam.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: