Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine na mtoto wa Museveni wajibizana vikali Twitter

Chadema Pic Bobi Wine Bobi Wine na mtoto wa Museveni wajibizana vikali Twitter

Fri, 20 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ama kweli maisha ni sanaa ya maigizo, baada viongozi wawili wa Uganda walioangaziwa katika mchoro wa katuni wakijibizana kufanya hivyo kiuhalisia.

"Kiatu hiki ni saizi yangu-usikaribie," mchoro unamuashiria kiongozi wa upinzani Bobi Wine akisema.

"Tulia Kaka! Sio kosa langu, ipo kwenye jeni yangu, "mwana mkubwa wa rais wa sasa wa Uganda alijibu katika mchoro huo wa katuni unaomuashiria.

Wahusika katika mchoro huo wa katuni wanajadiliana ni mguu wa nani utatoshea kwenye kiatu cha kiongozi wa Uganda aliyehudumu kwa muda mrefu Rais Yoweri Museveni, ambaye sasa ana umri wa miaka 77.

Mchoro huo ulishirikishwa kwenye mtandao wa Twitter na mwanawe rais Museveni Jenerali Kainerugaba.

Bobi Wine alimkosoa kwa kufikiria"Uganda ni moja ya mali ya baba yako ndio uwe mrithi"

Jenerali Kainerugaba, 47, amepanda madaraka kwa kasi katika jeshi la Uganda na kuna dhana kwamba anaandaliwa kuwa rais siku moja.

Amewahi kupinga dhana hiyo akisema kwamba Uganda sio"ufalme wa kisiasa"ambapo baba yake atamkabidhi hatamu za uongozi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live