Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bellingham atumika kumvuta Trent Madrid

Jude X Trent Bellingham atumika kumvuta Trent Madrid

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Taarifa za beki wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold kujiunga na Real Madrid katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi zimezidi kupamba moto, hususani baada ya kuonekana akiwa pamoja na staa wa mabingwa hao wa Hispania, Jude Bellingham kwa mara nyingine jijini Los Angeles, Marekani wiki hii.

Alexander-Arnold, ambaye ni nahodha msaidizi wa Liverpool kwa sasa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Liverpool na licha ya kufanya mazungumzo na mabosi wa timu hiyo hadi sasa bado hawajafikia muafaka.

Wakati muafaka ukiwa bado haujulikani taarifa zimeibuka kwamba Real Madrid inawinda huduma ya staa huyo na inamtumia Bellingham kama sehemu ya ushawishi kwa sababu ni rafiki yake wa karibu na wote wanaichezea timu ya taifa ya England.

Wawili hao ambao kwa sasa wapo mapumzikoni Marekani baada ya kupewa ruhusa ya kutokuwa katika kambi za timu zao kwa ajili ya maandalizi ya msimu kwa kuwa waliitumikia England katika michuano ya kimataifa, wamekuwa ni marafiki wa muda mrefu.

Real Madrid inaamini Bellingham na Trent ambao urafiki wao unadaiwa kuanza walipokutana kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa unaweza kuwa sababu tosha ya beki huyo kukubali ofa ya kujiunga na timu hiyo katika dirisha hili.

Hata hivyo, kama ikishindikana kumpata katika dirisha hili mabosi wa Real Madrid wamepanga kusubiri hadi mwisho wa msimu ujao kwa ajili ya kumsajili bure kama walivyofanya kwa Kylian Mbappe aliyejiunga nao katika dirisha hili akitokea PSG mkataba wake ulipomalizika.

Inaelezwa kwamba Liverpool inapambana kumshawishi Trent asaini mkataba mpya, lakini kama akikataa inaweza kumuuza ili asije kuondoka bure au kwa pesa kiduchu katika dirisha la majira ya baridi mwakani.

Chanzo: Mwanaspoti