Waziri wa Nishati, January Makamba amesema bei ya Dizeli kwa mwaka jana wakati wakisoma bajeti ilikua Sh. 3,452 na ikapanda mpaka Sh. 3,500 lakini kwasasa imeshuka hadi Sh. 2,800.
Makamba ameyasema hayo katika viunga vya Bunge jijini Dodoma kuongeza kuwa anatarajia mambo mazuri zaidi kwani kila asubuhi anapata ripoti ya mafuta yaliyopo, yanayotarajia kushushwa na yaliyopo kwenye meli.
Aidha, katika hatua nyingine Makamba amesema kutokana na mipango ya Serikali, ifikapo mwezi Juni mwaka 2024 vijiji vyote Tanzania vitakuwa na umeme.
Amesema Serikali ina mipango inayozingatia utabiri wa hali itakavyokuwa mbeleni, lakini pia inaishirikisha zaidi sekta binafsi katika kuwekeza kwenye sekta ya nishati, ili kuweza kufikia malengo kwa wakati.