Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barabara kufungwa kupisha kuadhimishwa siku ya kuzaliwa Rais Museveni

'Waganda Watajiendeleza Kwa Mikopo Au Bila'  Museveni Aijibu Benki Ya Dunia Barabara kufungwa kupisha kuadhimishwa siku ya kuzaliwa Rais Museveni

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barabara kadhaa zinatarajiwa kufungwa katika mji mkuu wa Uganda Kampala leo Ijumaa kwa ajili ya sherehe za kuadhimisha miaka 79 ya kuzaliwa kwa Rais Yoweri Museveni.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani jijini Kampala, Godwin Arinaitwe alitoa maagizo hayo kwa trafiki jana Alhamisi akisema tukio hilo litakalofanyika katika uwanja wa uhuru wa Kololo huenda likavutia wageni wapatao 100,000.

"Tunatarajia karibu wageni 100,000 ambao watakuja kutoka sehemu tofauti za nchi. Tunatoa wito kwa umma wa wageni kuwa waangalifu lakini pia kufuata miongozo ya trafiki,” Arinaitwe alinukuliwa.

Mkuu huyo wa polisi alisema barabara zinazotarajiwa kufungwa ni barabara ya Kololo Juu, Elgon na Kololo Chini ambazo zinahifadhiwa kwa ajili ya wageni wa hadhi ya juu.

Watumiaji wa barabara kutoka Barabara ya Bombo wameelekezwa kwenye Barabara ya Old Kira, Lugogo na kuegesha magari katika viwanja vya KCCA.

Kwa hiyo Kamanda huyo wa Polisi aliwataka watumiaji wa barabara katika mikoa iliyoathirika kufuata ushauri wa trafiki ili kuepusha usumbufu.

Sherehe hizo za kuzaliwa zinasemekana kuandaliwa na kundi la vijana, wakiongozwa na Mratibu wa Kitaifa katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha National Resistance Movement (NRM) Hadijah Namyalo.

Licha ya sherehe hiyo iliyopangwa kufanyika leo Septemba 8, siku ya kuzaliwa ya Rais Museveni itaangukia wiki moja baadaye Septemba 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live