Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam kumtangaza Mcolombia mwingine

Franklin Navarro Azam Azam kumtangaza Mcolombia mwingine

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Azam FC ni kama imenogewa na wachezaji kutoka Colombia, kwani kama mambo yatakwenda sawa, muda wowote watamtangaza beki kutoka nchini hiyo.

Hivi karibuni Azam FC ilimtangaza mshambuliaji Franklin Navarro (24) iliyemsajili kutoka Cortuluá FC ya Daraja la Pili ya nchini kwao, Colombia.

Habari kutoka ndani ya kikosi hicho, zinasema viongozi wanatarajia kumsainisha beki, huku jina lake likifichwa sana.

"Wanamalizana na beki raia wa Colombia na wanaweza wakamtangaza muda wowote kuanzia sasa, huyo atakuwa wa pili baada ya kumsainisha mshambuliaji Navarro," kimesema chanzo hicho.

Chanzo: Mwanaspoti