Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayewania kumrithi Fatma Karume TLS aikosoa Katiba

46350 Pic+wasonga Anayewania kumrithi Fatma Karume TLS aikosoa Katiba

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unatarajia kufanyika Aprili 6, 2019 Jijini Arusha, lakini mgombea wa nafasi ya urais, Godfrey Wasonga ameitaja Katiba ya Tanzania kuwa bado ina upungufu

Soma zaidi: Mambo matatu anayojivunia Fatma TLS

Wasonga ambaye anagombea kwa mara ya tatu sasa akiwania kumrithi Wakili Fatma Karume, amesema akipata nafasi ya kuongoza mawakili, ajenda yake kubwa itakuwa ni kufanya ushawishi kwa viongozi ili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifanyiwe mabadiliko.

“Hatuwezi kuzungumzia demokrasia kama Katiba ina upungufu ndani yake, lazima sisi wanasheria tuzungumze na kukubaliana na wasomi, wanazuoni na jamii kwa nia njema ya kupata kitu kizuri,” amesema Wasonga.

Mgombea huyo pia amemmwagia sifa Tundu Lissu akisema kuwa aliongoza na kuifanyia marekebisho makubwa TLS na kuongeza kuwa kama Lissu angepewa nafasi hiyo kwa muda zaidi huenda wangekuwa mbali zaidi.

Wakili huyo amesema kuwa uongozi wa Lissu aliyeshika nafasi hiyo kabla ya Fatma, unatakiwa kufuatwa na viongozi wanaoingia ndani ya TLS na kuboresha zaidi ndipo watafikia mafanikio.

Soma zaidi: Sita wawania kumrithi Fatma Karume TLS

“Lissu alituongoza vizuri sana, mimi nakubali uongozi wake isipokuwa tunatofautiana kwenye matusi na kejeli zake ndani ya Serikali, lakini lazima tukubali kuwa jamaa alifanya kazi nzuri sana yenye mfano wa kuigwa,” amesema.

Wasonga pia amesema kwamba akishinda na kuwa Rais wa TLS atakifanya chama hicho kuwa cha uwekezaji kwenye ardhi na atahamisha mikutano ambayo kila wakati inafanyikia Arusha ili kupeleka mikoani ambako gharama zitakuwa ndogo.

Soma zaidi: Lissu atumikia urais TLS kwa miezi sita tu, kuondoka Aprili



Chanzo: mwananchi.co.tz