Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Mukwala ana uwezo mkubwa wa kufunga

Mukwala Mszh Ahmed Ally: Mukwala ana uwezo mkubwa wa kufunga

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa uwezo wa kufunga wa mshambuliaji wao, Steven Mukwala raia wa Uganda ni mkubwa kuliko watu wanavyomdhania.

kauli hiyo ya Ahmed inakuja huku kukiwa na taarifa kubwa Simba wanatafuta mshambuliaji mwingine baada ya Mukwala aliyesajiliwa msimu huu akitokea Asante Kotoko ya Ghana kuonekana hajakidhi ubora unaotakiwa na Wanasimba.

"Ana kila kitu cha Mshambuliaji Bora, Makadirio (Antacipation) yake ni ya hali ya juu, Pressing yake kwa mabeki ni ya kiwango cha juu , dribbling yake akiwa na mali ni nzuri.

"Kilichobaki ni kimoja tuu kufunga na Uwezo wake wa kufunga hauna shaka ila anahitaji muda kidogoo.

"Jukumu letu ni kuendelea kumpa moyo kwani haina ubishi Mukwala ni Mshambuliaji mzuri na muda si mrefu ataaanza kufanya Ubaya Ubwela," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live