Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuchu adaiwa kumpiga chini tena Diamond, asepa na mabegi yake

Zuchu Afunguka Kumbebea Diamond Mimba Mwaka Huu.png Zuchu adaiwa kumpiga chini tena Diamond, asepa na mabegi yake

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dada wa msani wa muziki Diamond Platnumz "EsmaPlatnumz" amedai kuwa Mpenzi wa mdogo wake "Zuchu" amebeba mabegi yake na kuondoka nyumbani.

Zuchu anadaiwa kufanya uamuzi huo baada ya Diamond Platnumz kumpandisha mwanamke mwingine kwenye steji kwenye show yake ya weekend iliyopita na kumuita jina la Ex wake 'Sarah!.

Kwa mujibu wa Diamond Platnumz ni kwamba Sarah ndiye mwanamke ambaye alitokea kumpenda kuliko wanawake zake wote aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano.

Aidha, Esma amemuomba Zuchu arudi nyumbani kwani mwanamke huyo aliyemwita stejini ni Ex tu wala sio kama anavyofikiri yeye.

Sarah ndiye aliyemfanya aandike wimbo wake wa (Nenda kamwambie) ambao ndio ulikuwa wimbo wa kwanza kumtoa na kumfanya ajulikane kimataifa, lakini wimbo huo uliandikwa mahususi kwa ajili ya kumuomba msamaha Sarah ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na uzuri wa ajabu mithiri ya kuku kinyanyoke.

"Huyu ndiye Sarah wa miaka 15 nyuma, nilimpenda sana, nilimwimbia wimbo wa 'Nenda Kamwambie' kipindi hicho nikimwona nachanganyikiwa. Kilichomo kwenye ule wimbo ni sababu yake. Baadaye tulikutana tukazungumza tukayamaliza," alisema Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: