Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto: Nchi zisizopenda Demokrasia zinapenda kwenda China

Zitto Pic Zitto: Nchi zisizopenda Demokrasia zinapenda kwenda China

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa na Mchumi, Zitto Kabwe amesema kuwa Mataifa ya Kiafrika ambayo hayazingatii misingi ya kidemokrasia katika utawala ujifungamanisha zaidi na China kwa kuwa Taifa hilo halina utamaduni wa kuhoji juu ya masuala mbalimbali yanayofungamana na haki za binadamu.

"China wanavyosaidia Nchi zetu hawajali haya mambo ya Haki za Binadamu, hawajali maswala ya kidemokrasia wao wanachoangalia ni kwamba watapata faida gani na hiyo Nchi itapata faida gani, kwahiyo kwa mahusiano kama haya Nchi ambazo ni za kidikteta zisizopenda demokrasia, watawala wake wasiopenda kuhojiwa wanapenda zaidi kujiunganisha na China, kwa sababu China haitauliza"

Amesema utaratibu huo upelekea wananchi kuumia, kutokana na masuala ya haki za binadamu kutofungamanishwa na misaada ambayo utolewa au viongozi kutohojiwa kutokana na misaada ambayo utolewa.

"Katika mazingira kama hayo wanaoumia hasa ni raia wa kawaida wa Mataifa hayo ambayo Serikali zao au watawala wao hawawezi kuhojiwa na Watu ambao wanawapa misaada kwa maana uwa tunasema"

Ameyasema hayo katika mjadala wa Meza ya Duara (DW) ambapo ulikuwa ukijadili na kutathimini Mkutano baina ya Afrika na China ambao umefanyika Septemba 4 hadi 6, 2024 nchini China kwa kuwakutanisha baadhi ya viongozi wa Mataifa ya Afrika, ambapo mjadala uligusia masuala mbalimbali ikiwemo ya kisera na kiuchumi.

Aidha akizungumza katika mjadala huo amesema kwa deni la China kwa mataifa ya Afrika ni asilimia 12 ya madeni yote ya Kimataifa, ambapo kwa nchini Tanzania katika deni la Taifa asilimia 9 ni la China.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live