Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Simbachawene kaagiza kusakwa wote wanaomchafua Rais Samia

Ewew George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. George Simbachawene, ameelekeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini kuwatafuta watu wote wanaowachafua wenzao mitandaoni hasa wanaomdhihaki Rais wa Tanzania na serikali na hatua kali zifuatwe na kuwafikisha mahakamani kwa haraka.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo mapema leo September 16, 2021 makao makuu ya Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba Dodoma wakati akizungimza na viongozi wa idara zote za ulinzi na usalama nchini ambapo ameelekeza kufanyike msako wa haraka kuwabaini watu hao na kuwakamata kwakua kumeibuka tabia ya watu kutumia vibaya mitandaoni hiyo kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameagiza msako wa wezi mitandaoni kwa kuwa inakadiriwa kuwa kwa siku milioni 500 zinakua kwenye wizi wa kimatandao huku akikataza wananchi kutoa fedha kwa ajili yakufuatilia polisi taarifa za simu zao zilizoibiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live