Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mkuu Majaliwa anena kuhusu Rais Magufuli

Etrtrt 660x400 Waziri Mkuu Majaliwa anena kuhusu Rais Magufuli

Sat, 13 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana, kudumisha amani na wapuuze kauli za chuki zinazotolewa na watu wasioitakia mema nchi kuhusu afya ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani ni mzima wa afya.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana, kudumisha amani na wapuuze kauli za chuki zinazotolewa na watu wasioitakia mema nchi kuhusu afya ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani ni mzima wa afya. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Machi 12, 2021) baada ya kushiriki sala ya Ijumaa mjini Njombe, ambapo amesisitiza kuwa Rais anafanya kazi kulingana na mpango kazi wake. Amesema wananchi wanatakiwa kushikamana na kuifanya nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu.

Chanzo: millardayo.com