Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Kakunda aeleza alichozungumza mara ya mwisho na Mengi

55290 KAKUNDA+PIC

Fri, 3 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia leo atakumbukwa kwa mengi nchini hasa kuwa kinara kwenye sekta ya biashara na viwanda, huku akidokeza alichozungumza mara ya mwisho na mfanyabiashara huyo.

Mengi amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Alhamisi Mei 2 akiwa Dubai.

Waziri Kakunda ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora alitoa kauli hiyo wakati akizungumza jana na Mwananchi na kusema Mengi alianza kuwa kinara kwenye sekta ya biashara na viwanda tangu enzi za Azimio la Arusha hadi sasa.

 “Mengi amekuwa kiongozi wa wenye viwanda, wafanyabiashara, mwekezaji, mmiliki wa viwanda na biashara mbalimbali, mmiliki wa vyombo vya habari na pia mwalimu wa wajasiriamali Tanzania na Afrika Mashariki.” 

 “Amefariki akiwa na ndoto ya kuendelea kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kuanzia madini hadi usindikaji wa mazao ya kilimo na pia viwanda vya simu, TV na magari,” alisema Kakunda.

Waziri huyo alisema mara ya mwisho alizungumza na Mengi Februari mwaka huu  kuhusu mkopo aliokuwa akiutaka kutoka TIB Corporate Bank. “Na nilimuhakikishia kuwa namsapoti.”

Alisema lengo la mkopo huo lilikuwa uwekezaji kwenye mradi wa kuunganisha mabasi.

Kakunda alitumia nafasi hiyo kutoa salamu za pole kwa familia yake na Watanzania na kusema taifa linapaswa kumuenzi kishujaa kwa kuthamini mchango wake na pia kusaidia maendeleo ya viwanda na biashara nchini.



Chanzo: mwananchi.co.tz