Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto sita waliokufa Rorya wazikwa

Watoto 47 Facebook Watoto sita waliokufa Rorya wazikwa

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miili ya Watoto 6 wanafunzi wa Shule ya Msingi Ochuna, waliofariki dunia kwa kuzama na kunasa kwenye tope katika Bwawa la Skimu ya umwagiliaji wa Kijiji cha Ochuna, Wilaya ya Rorya mkoani Mara, inaagwa na kuzikwa jana katika eneo la viwanja vya Shule ya Msingi Ochuna.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa pole na rambirambi ya Tsh milioni 30 kufuatia vifo vya Watoto hao ambao wote ni Wasichana.

Akiwasilisha rambirambi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka amesema kwa mujibu wa Rais Samia, fedha hizo zimetolewa kwa kila Familia ya Mtoto aliyefariki dunia, ambapo kila Familia itapata Tsh. milioni tano.

Jana miili hiyo iliagwa na Watoto wanne watazikwa eneo moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live