Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wastaafu ACT-Wazalendo kupewa usafiri na nyumba

ADO SHAIBU Wastaafu ACT-Wazalendo kupewa usafiri na nyumba

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT Wazalendo kinamuaga aliyekuwa mwenyekiti wake Juma Duni Haji (Babu Duni) ikiwa ni utekelezaji wa sera yake mpya ya kuwaenzi viongozi wake wastaafu. Ikumbukwe kuwa Babu Duni aliachia ngazi mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud.

ACT Wazalendo wameweka sera maalum ya kuwaenzi wastaafu wake na wanaohusika ni kiongozi wa chama mstaafu na mwenyekiti wa chama mstaafu.

Akizungumza katika tukio hilo Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu amesema kuwa sera hiyo iliwekwa ili kuwalinda na kuwajali viongozi wake wastaafu huku akisema chama hicho ndio chama pekee Tanzania kinachofanya hivyo.

"Sera imeweka utaratibu wa kuwajali, kuwaangalia, na kuwatunza viongozi wakuu wastaafu na imeweka mazingira ya namna mbili, wapo viongozi wawili wametajwa kwenye sera ile, Kiongozi wa Chama mstaafu, na Mwenyekiti wa chama mstaafu, hawa ni lazima kuwaangalia, kuwajali.

"Sera imeweka utaratibu wa kuwajali, kuwaangalia, na kuwatunza viongozi wakuu wastaafu na imeweka mazingira ya namna mbili, wapo viongozi wawili wametajwa kwenye sera ile, Kiongozi wa Chama mstaafu, na Mwenyekiti wa chama mstaafu, hawa ni lazima kuwaangalia, kuwajali n#eastafricatva kuwatunza.

"Na zipo stahiki zimewekwa kwenye sera ile na inasema iwapo kiongozi wa chama mstaafu na mwenyekiti wa chama mstaafu watakuwa hawana makazi ni wajibu wa chama kuhakikisha wanapata makazi, na iwapo watakuwa hawana usafiri unaoendana na hadhi ya Kiongozi wa chama mstaafu na mwenyekiti wa chama mstaafu ni wajibu wa chama kuhakikisha viongozi hawa wanapata usafiri, na sera inasema tuwaangalie pia kwenye matibabu na mambo mengine ya kimaisha," amesema Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT Wazalendo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live