Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiojulikana waua mmoja, wajeruhi mke, watoto

George Katabazi .png Wasiojulikana waua mmoja, wajeruhi mke, watoto

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wasiofahamika wamemuua mkazi wa Dodoma Michael Richard (26), mkewe na watoto wawili wamejeruhiwa na nyumba waliyokuwa wakiishi imechomwa moto.

Waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ni mke wa Michael, Agnes Eliah na watoto Ezra Michael, Witness Michael, Ephrahim Michael na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ambaye yeye aliathiriwa na moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi alisema tukio hilo limetokea Agosti 28 saa 9:00 alfajiri. Kamanda Katabazi alisema uchunguzi wa awali unaonesha Michael alivamiwa nyumbani kwake eneo la mtaa wa Mbuyuni, kata ya Kizota na kuuawa kwa kupigwa kichwani na kitu chenye ncha butu.

“Baada ya tukio hilo walichoma moto godoro lakini inaonekana huyu mtu alishauawa na badaaye kuwashambulia na kuwajeruhi watoto wawili na mke wake,” alisema. Aliongeza, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipa kisasa ingawa alisema bado hawajajua kisasi hicho kilichangiwa na nini.

“Kwa sasa vijana wanaendelea na uchunguzi mkali na bado hatujajua hasa kisasi hicho kilitokana na nani. Tunaendelea na msako mkali na tunaamini tutafanikiwa kuwakamata,” alisema na kuongeza kuwa wahalifu hao walichoma moto godoro ili kupoteza mazingira ya ushahidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live