Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waombolezaji wachafukwa, wakatisha hotuba ya Waziri Masauni, wamtaka aondoke msibani

Masauni MAI7jPM.jpeg Waombolezaji wachafukwa, wakatisha hotuba ya Waziri Masauni, wamtaka aondoke msibani

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vurugu imetokea wakati hotuba zikiendelea katika msiba wa aliyekuwa kada wa Chadema, Ali Kibao nyumbani kwake mkoani Tanga, wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akihutubia wananchi.

Kelele hizo zimeibuka zikimtaka Waziri Masauni kujiuzulu nafasi yake kutokana na matukio ya kutekwa wananchi yanayoendelea nchini.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwatuliza wananchi hao na kuwaomba kumuacha Waziri Masauni kumaliza hotuba yake na alifanikiwa kumaliza hotuba hiyo.

Kibao anatarajiwa kuzikwa leo Jumatatu Septemba 9, 2024, saa 7 mchana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live