Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wanusurika kuuawa wakidhaniwa kuwa ni watekaji wa watoto

IMG 20240831 WA0005 Wanne wanusurika kuuawa wakidhaniwa kuwa ni watekaji wa watoto

Sat, 31 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wamenusurika kifo baada ya kupigwa na kukatwa mapanga pamoja na gari waliyokuwa wakiitumia aina ya Raum kuchomwa moto katika Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara kwa kudhaniwa kuwa ni wezi wa kuiba Watoto baada ya kumpa pipi Mtoto aliyekuwa akipita pembeni ya gari yao waliyokuwa wanaitumia.

Neema Kilai ambaye alikuwa kwenye gari hiyo amesema kuwa walikuwa wakitoka kwenye harusi katika kijiji cha Kidarafa katika shughuli ya kupika ambapo gari yao ilipata pancha ghafla waliona gari yao ikiwa imezungukwa na walipofika pale waliambiwa kuwa wao ndio wanahusika kuwakata Watoto viungo.

Amesema kuwa Wananchi hao wakiongozwa na baadhi ya Viongozi walianza kuwashambulia kwa mapanga na mawe na kisha baadaye kuanza kuichoma gari hiyo.

“Kwenye gari tulikuwa tumebeba mahindi, jogoo wawili tumepewa, kuna njiwa, kuna begi zetu na nyama, pipi zilikuwa za kwetu tulikuwa tumenunua tunatafuna, Mtoto alivyopita akatuona tunakula yule rasta akampa kidogo Mama yake akatokea akawa anamchapa yule Mtoto yule wifi wangu akauliza mbona unamchapa Mtoto hivyo?akamuambia haikuhusu wakaanza kuongezeka, walituambia tuvue nguo zote ila Kaka yangu akasema kuliko nivue bora mniue,” amesema Neema.

Watu wawili kati ya wanne wametibiwa katika Hospitali ya Meru lakini wengine wawili ambao ni Mke na Mume wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live