Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wageni 204 wapewa uraia wa Tanzania

BAJETI MASAUNI Wageni 204 wapewa uraia wa Tanzania

Tue, 30 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu wa 2023 jumla ya Wageni 204 walikuwa wamepewa Uraia wa Tanzania huku idadi hiyo ikiizidi ile ya mwaka 2021/2022 ambayo ilikua ni Wageni 112.

Waziri Masauni ameyasema haya leo Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema Wageni hao 204 ni kutoka Mataifa haya 22, Afrika Kusini Wageni watatu (3), Cameroon Mgeni mmoja, China Wageni wawili (2), Cuba Mgeni mmoja (1), DRC Wageni 11, India Wageni 75, Japan Mgeni mmoja (1), Kenya Wageni 12, Lebanon Wageni 10, Lithuania Wageni wawili (2), Oman Mgeni mmoja (1).

Pakistani ni Wageni 22, Palestina Mgeni mmoja (1), Rwanda Wageni wanne (4), Sierra Leone Mgeni mmoja (1), Somalia Wageni wanne (4), Ugiriki Wageni wawili 2, Uingereza Wageni wawili 2, Uswizi Wageni wawili (2), Yemeni Wageni 43, Zambia Wageni wawili (2) na Zimbabwe Wageni wawili (2).”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: