Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafia kwa mganga kisa kuboost biashara

Kifo Mautii Wafia kwa mganga kisa kuboost biashara

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi linawashikilia Mtila Ausi maarufu Shehe Mtila (Mganga wa kienyeji), Omary Abdallah na Amini Sanga kufuatia vifo vya Wafanyabiashara wawili Mkoani Ruvuma ambao ni Raymond Hyera na Riziki Mohamed waliofika kwa Mganga huyo ili kupata dawa za kuwawezesha biashara zao kufanya vizuri zaidi na wakapewa maji yaliyowafanya walegee na kufariki na kisha wakazikwa kimyakimya.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime September 04,2024 imesema “August 03, 2024 katika Kituo cha Polisi Songea Mkoa wa Ruvuma, zilipokelewa taarifa za kupotea kwa Wanyabiashara wawili toka July 31, 2024, Wafanyabiashara hao walitajwa na Ndugu waliofika kituoni kutoa taarifa kuwa ni Raymond Hyera jina maarufu Ray (25) Mkazi wa eneo la Msamala, Manispaa ya Songea na Riziki Mohamed (30) Mkazi wa eneo la Mjimwema, Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma”

“Baada ya uchunhuzi na mahojiano, Mganga na wenzake walikiri Wafanyabiashara hao kufika nyumbani kwao wakiambatana na Mfanyabiashara menzao aitwaye Amini Sanga kwa lengo la kupata dawa za kuwawezesha biashara zao kufanya vizuri zaidi, waliwanywesha maji ambayo yaliwafanya walegee na kupelekea kupoteza maisha, baada ya kufariki, waliwachukua na kwenda kuwazika katika pori la Mdinguli, kijji cha Mtangashari, Tunduru kisha kuchukua fedha walizokuwa nazo Tsh. milioni ishirini na kugawana”

“September 03, 2024, Mtila Ausi na Omary Abdallah waliwaongoza Polisi hadi walipowazika Wafanyabiashara hao, ufukuaji ulifanyika na miili ya Wafanyabiashara hao ilikutwa, uchunguzi unaendelea kukamilishwa ukiwepo wa kisayansi ili taratibu nyingine zifuate”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live